Kuhusu kanisa

Kanisa la familia, ibada, uanafunzi, na mguso kwa jamii.

TAG-CICC ni kanisa la kipentekoste chini ya Tanzania Assemblies of God, likihudumia watu wa rika mbalimbali kupitia ibada, idara, kanda, maombi, uinjilishaji, na huduma za kijamii.

Familia na viongozi wa TAG-CICC wakiwa pamoja
TAG-CICC

CITY IMPACT CHRISTIAN CENTRE

Tunajenga mazingira ya kiroho na kiutendaji yanayowawezesha washirika kumjua Kristo, kukua katika imani, na kushiriki kwenye huduma zinazogusa familia na jamii inayotuzunguka.

Dhamira yetu

Kumhubiri Kristo, kulea waamini, na kuwaandaa washirika kumtumikia Mungu kwa uaminifu katika kanisa na jamii.

Maono yetu

Kuwa kanisa linaloleta mguso wa Kristo kwa jiji na jamii kupitia ibada, uanafunzi, na huduma zenye matokeo.

Tunachokithamini

Neno la Mungu, maombi, ushirika, uaminifu, uwajibikaji, huduma, na upendo kwa watu wote.